• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda Mapato ya nje ya chai imeongezeka hadi Rwf bn 19.4 katika robo ya kwanza

    (GMT+08:00) 2017-05-31 20:04:32

    Rwanda ilipata zaidi ya dola milioni 23 kutokana na mauzo ya nje ya chai katika robo ya kwanza ya mwaka, ambayo ni ongezeko kutoka dola milioni 18.9 iliyorekodiwa katika mwaka wa 2016, ripoti ya Bodi ya Taifa ya mauzo ya nje ya Kilimo (NAEB) inaonyesha.

    Shirika la mauzo ya nje limesema ongezeko hili limechangiwa na bei nzuri katika miezi ya kwanza mitatu 2017.

    Maafisa wa NAEB wanasema mapato iliyotengenzwa katika robo ya kwanza ilizidi makadirio.

    Mauzo ya nje ya chai nchini Rwanda ilikuwa yenye thamani dola milioni 6.6 mwezi Machi, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

    Jumla ya mapato ya mauzo ya nje nchini Rwanda ilifikia dola milioni 558.8 mwaka jana.

    Hata hivyo shirika la mauzo ya nje linatafuta masoko mapya kwa ajili ya chai ya Rwanda ili kuongeza mauzo ya nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako