• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Borussia Dortmund yamtimuwa Thomas Tuchel baada ya kuipatia kombe la Ujerumani

    (GMT+08:00) 2017-06-01 09:29:27

    Borussia Dortmund imemtimua kocha wake Thomas Tuchel siku tatu tu baada ya kuiongoza klabu kupata taji lake la kwanza katika miaka mitano.

    Klabu hiyo ilitoa taarifa ikisema Tuchel mwenye miaka 43 anaondoka mara moja klabuni hapo akiwa bado amesaliwa na mwaka mmoja klabuni kulingana na mkataba wake unaokwisha muda mwaka 2018. Mechi ya mwisho aliyoongoza Tuchel waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt kwenye hatua ya fainali ya kombe la Ujerumani iliyochezwa Jumamosi.

    Tuchel, kocha wa zamani wa Mainz ambaye amefuata nyayo za Juergen Klopp kuifundisha Dortmund mwaka 2015, ameipeleka timu katika nafasi ya pili kwenye Bundesliga msimu wake wa kwanza, na hatua ya fainali ya Kombe la Ujerumani, ambapo hatimaye ilishindwa na Bayern Munich.

    Mgogoro wa Tuche na Dortmund ulianzia tangu januari 2016 wakati alipochafuana na Sven Mislintat, kwa kumsaini kiungo wa kati Oliver Torres kutoka Atletico Madrid.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako