• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbiaji wa Kenya waendeleza ubabe wao Marathon ya Ningxia Yinchuan China

    (GMT+08:00) 2017-06-01 09:29:48
    Mbio za kwanza za kimataifa za Marathon ya Ningxia Yinchuan zilianza kutimua vumbi katika mji wa Yinchuan jumapili hapa China, huku wakimbiaji wa Kenya wakiendeleza ufahari wao kwenye mbio ndefu kwa kushinda mataji ya wanawake na wanaume.

    Bethwel Biwott Yegon amebeba taji kwa upande wa wanaume baada ya kukimbia kwa saa 2:24:00, huku Cheboi Consolata Jepkosgei akinyakua la wanawake kwa kutumia muda wa saa 2:54:15.

    Kwa mujibu wa wandaaji, mbio hizo zilijumuisha marathon, nusu marathon marathon ndogo, na kushirikisha wakimbiaji 20,000 kutoka nchi na kanda 41, ikiwemo Kenya, Marekani, Ufaransa, Denmark na Albania.

    Wakimbiaji wa kiume kutoka Kenya wamezoa nafasi tatu za juu huku Lu Chunyang na Mei Ying, kutoka China, wakikamata nafasi ya pili na tatu kwa upande wa wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako