• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yathibitika: Arsene Wenger bado yupo klabuni Arsenal

    (GMT+08:00) 2017-06-01 09:30:09

    Baada ya klabu ya Arsenal kutokuwa na mwenendo mzuri katika kipindi cha hivi karibuni, mashabiki wengi wa timu hiyo walishinikiza Kocha Arsene Wenger afukuzwe, hususan baada ya kukosa nafasi ya kushiriki Ligi ya mabingwa.

    Arsenal itakosa kushiriki Ligi ya mabingwa msimu wa 2017/2018 kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki katika michuano hiyo kwa miaka 20 mfululizo, hivyo kutokana na kushuka huko wengi walikuwa wanahisi Wenger atafukuzwa. Lakini jana uongozi wa klabu ya Arsenal ulithibitisha kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili.

    Wenger atadumu ndani ya Arsenal hadi mwaka 2019, maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka Wenger aipe Arsenal Ubingwa wa 13 wa FA kwa kuifunga Chelsea na kuifanya kuwa klabu pekee iliyotwaa taji hilo mara nyingi zaidi ikifuatiwa na Man United.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako