• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester United yatajwa kuwa Klabu yenye thamani zaidi 2017

    (GMT+08:00) 2017-06-01 09:41:03

    Washindi wa Europa League msimu wa 2016/17 Manchester United ya England imetajwa kuwa Klabu yenye thamani zaidi 2017 ikizipiku miamba ya La Liga Real Madrid na Barcelona zilizokamata nafasi ya pili na tatu.

    Katika utafiti uliohusisha bei za matangazo, faida inayopatikana kwa mwaka, umaarufu, uwezo wa kimchezo na umiliki wa uwanja miongoni mwa klabu 32 za Ulaya, United imeibuka kinara kwenye orodha hiyo ikiwa na thamani ya euro bilioni 3.09.

    Nafasi ya pili inakamatwa na mabingwa wa La Liga Real Madrid yenye thamani ya euro bilioni 2.97 huku Barcelona wakichukua nafasi ya tatu wakiwa na thamani ya euro bilioni 2.76, ambapo katika kumi bora za Uingereza imeingiza klabu Sita ikifuatiwa na Hispania yenye timu Mbili huku Ujerumani na Italia zikiwa na klabu moja moja kila nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako