• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na Chansela wa Ujerumani

    (GMT+08:00) 2017-06-01 10:06:54

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang jana mjini Berlin alikutana na Chansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel.

    Bw Li Keqiang amesema uhusiano kati ya China na Ujerumani unaendelea kwa kasi, pende zote mbili zinatakiwa kuheshimiana, kuimarisha uaminifu, kuzidisha ushirikiano na mawasiliano. Amesema China na Ujerumani zina mustakbali mkubwa wa ushirikiano, na China inapenda kuzidisha ushirikiano na Ujerumani katika uzalishaji viwandani, nishati, usafiri wa anga, uvumbuzi, mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati. Pia amesisitiza kwamba China na Umoja wa Ulaya ni wenzi wa kimkakati wa pande zote, na inauunga mkono mafungamano ya nchi za Ulaya.

    Kwa upande wake Bibi Merkel amesema Ujerumani ni mwenzi wa kuaminika wa China, na inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na China katika sekta za biashara, uwekezaji, fedha, magari yanayotumia nishati mpya, afya na utamaduni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako