• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Serikali ya Uganda kuhamisha viwanda vya sukari

    (GMT+08:00) 2017-06-01 19:04:47

    Serikali ya Uganda inapanga kuhamisha viwanda vya sukari vya GM Sugar na Mayuge Sugar kutoka eneo la mashariki mwa nchi hiyo ili kupunguza upandaji wa miwa ambao serikali inataja kama sababu ya kuwa na njaa, umaskini na uharibifu wa mazingira.

    Waziri wa maswala ya jamii ya Karamoja Moses Kizige amesema wakulima wengi katika eneo la Busoga wanaendelea kupunguza uzalishaji wao wa mimea ya chakula na kutumia mashamba yao kuzalisha miwa.

    Alisema wakulima wengine pia wanakondisha mashamba yao kwa pesa ndogo ili yatumiwe kupanda miwa.aidha waziri huyo alisema serikali itaanza kutekeleza sera mpya ya sukari iliopitishwa na baraza la mawaziri kwa lengo la kuzuia wakulima kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji na ukataji miti.

    Kampuni zitakazohamishwa zitapewa fidia na serikali na pia hazitalipa kodi kwa miaka 5.

    Eneo la Busoga kwa sasa lina viwanda 5 vya sukari vikiwemo Kakira, Mayuge na GM.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako