• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Benki ya Dunia yashauri serikali ya Tanzania kuwekeza katika Bonde la Msimbazi

    (GMT+08:00) 2017-06-01 19:06:49

    Benki ya Dunia (WB) imeishauri serikali kuwekeza katika Bonde la Msimbazi ili kuepusha mafuriko ambayo yamekuwa yakichukua maisha ya watu na kuharibu makazi na miundombinu muhimu.

    Akiwasilisha hoja katika mkutano wa wadau, mtaalamu mwandamizi wa Tehama na udhibiti wa maafa hatarishi, Edward Anderson amesema uwekezaji huo ujikite katika kuangalia gharama za kuzuia maafa na gharama za kukarabati uharibifu unaosababishwa na maafa hayo.

    Anderson amesema mji wa Dar es Salaam ni muhimu kwa sababu asilimia 40 ya Pato la Taifa (GDP) linapatikana hapa, hivyo lazima serikali ihakikishe kwamba inajenga miundombinu mizuri katika bonded hilo ili kuondoa uharibifu unaosababishwa na mafuriko.

    Amesema bonde la msimbazi linaweza kuongezewa matumizi mbali ya kupitisha maji pekee. Ametaja matumizi hayo ni pamoja na kujengwa kwa bustani ya wazi na kilimo cha umwagiliaji katika bonde hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako