• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema uzinduzi wa Reli ya SGR ni mafanikio ya urafiki na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Kenya

  (GMT+08:00) 2017-06-01 19:33:56

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, uzinduzi wa Reli ya SGR ni mafanikio ya urafiki na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Kenya, huku akisisitiza kuwa China ni rafiki halisi na mwenzi wa maendeleo wa kutegemewa wa Afrika.

  Bibi Hua amesema, katika ujenzi wa reli hiyo, kampuni ya China ilifuata kanuni za kulinda mazingira ya kimaumbile, kuhakikisha mazingira ya kimaumbile kando ya reli hiyo hayaharibiwi, na kulinda mimea na wanyamapori.

  Pia amesema, China inapenda kufanya juhudi pamoja na Kenya kuimarisha ujenzi wa maeneo ya viwanda yaliyo kando ya reli hiyo, kujenga ushirikiano mpya kati ya reli ya SGR, bandari ya Mombasa na eneo maalumu la kiuchumi la Mombasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako