• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kutangaza kujitoa makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2017-06-02 08:52:08

    Rais Donald Trump wa Marekani jana alitangaza rasmi kuwa Marekani itajitoa kwenye makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

    "Kuanzia leo hii, Marekani itasimamisha utekelezaji wa makubaliano ya Paris yasiyo na nguvu ya kisheria. "

    Baada ya Trump kutoa kauli hiyo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa taarifa akisema Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya Paris ni jambo la kusikitisha kwa juhudi za dunia nzima katika kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni, na kuhimiza usalama wa dunia.

    Viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Italia walitoa taarifa ya pamoja kueleza kusikitishwa kwao na uamuzi wa Marekani, na kusema zitaendelea kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa makubaliano hayo.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto inayoikabili dunia nzima, hakuna nchi yoyote inayoweza kukwepa, na China itaendelea kuwa mlinzi na mhimizaji wa usimamizi wa hali ya hewa, duniani na kujitahidi kushiriki kwenye mchakato wa pande zote wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Sekretariati ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ya UNFCCC imetoa taarifa ikisema, makubaliano ya Paris ni mkataba unaosainiwa na nchi 194 na kuidhinishwa na nchi 147, na hayatajadiliwa upya kwa mujibu wa matakwa ya upande mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako