Wizara ya miundombinu ya Rwanda imesema Rwanda inatafuta wawekezaji wa nje na wa ndani kwenye sekta ya nyumba za bei nafuu kutokana na ongezeko la watu wa mjini.
Nyumba za bei nafuu ni moja ya malengo ya mpango makini wa maendeleo ya miundombinu kwenye sekta ya makazi ya mjini na ya vijijni nchini Rwanda.
Mkutano kwa ajili ya maendeleo ya nyumba za bei nafuu ulifanyika jana mjini Kigali, kwa lengo la kuweka fursa kwa wadau na mashirika ya fedha katika soko la nyumba.
Kwenye mkutano huo waziri wa miundombinu wa Rwanda Bw James Musoni amesema Rwanda bado iko katika hatua za awali kwenye uwekezaji wa nyumba za bei nafuu zinazoweza kuwanufaisha watu wenye mapato ya chini na ya kati. Amesema Serikali itawapatia wawekezaji ardhi ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo, ili kuwawezesha wananchi wake wa mijini waishi katika nyumba hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |