• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taifa stars yaanza kujinoa dhidi ya Lesotho nchini Misri

    (GMT+08:00) 2017-06-02 11:20:29

    Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania, Taifa stars imeanza kujifua kwa mazoezi mazito kuanzia usiku wa juzi mara tu baada ya kufika salama mjini Alexandria, nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki moja. Akizungumza mara baada ya mazoezi hayo Kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga amesema waliridhika na viwanja vya mazoezi baada ya kuvikagua na moja kwa moja jioni hiyo kuanza progaramu ya mazoezi.

    Kocha Mayanga ambaye alipewa majukumu ya kuifundisha timu hiyo mapema Januari, mwaka huu, amesema programu ya mazoezi kwa timu itakuwa zaidi usiku kwa sababu mchezo wao dhidi ya Lesotho pia utachezwa usiku, hii ni kutokana na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ingawa wakati mwingine mazoezi yatafanyika asubuhi na jioni.

    Taifa Stars kwa sasa inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku. Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi 'L' kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako