• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazidi kujiimarisha kwenye viwango vya soka vya FIFA

    (GMT+08:00) 2017-06-02 11:20:48

    Kenya imepaa nafasi nne hadi nafasi ya 74 duniani katika viwango bora vya Shirikisho la Soka duniani FIFA vilivyotolewa jana Alhamisi.

    Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane na miezi sita kwa Kenya kufikia mojawapo ya nafasi yake bora katika viwango hivyo.

    Ufanisi huo umepatikana baada ya Harambee Stars kudumisha rekodi ya kutoshindwa mechi 11 katika kipindi cha miezi 13.

    Uganda inaongoza viwango hivyo katika eneo la Afrika Mashariki na Kati Cecafa. Inashikilia nafasi ya 71 duniani baada ya kuimarika na nafasi moja. Ethiopia nayo iko chini kwa nafasi moja hadi 125 duniani, Rwanda imeteremka nafasi 10 hadi 128 duniani, na Tanzania imetupwa chini nafasi nne hadi 139 duniani.

    Misri inaongoza msimamo wa Afrika katika nafasi ya 20. Imeteremka nafasi moja. Ikifuatiwa na Senegal nafasi tatu juu hadi 27 duniani, mabingwa wa Afrika Cameroon wapo nafasi moja juu hadi 32 duniani, huku Nigeria ikiimarika nafasi mbili hadi 38 duniani, DR Congo ipo nafasi mbili juu hadi 39 duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako