• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gianluigi Buffon aahidi kutoirusuhu Real kutingisha nyavu zao kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-06-02 11:21:57

    Mlinda mlango wa Juventus Gianluigi Buffon, mwenye miaka 40 sasa ameahidi kutumia tajriba yake na nguvu zake zote kuhakikisha anazuia makombora ya washambuliaji wa Real Madrid timu hizo mbili zitakapokutana Jumamosi katika mchuano mkali wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.

    Buffon amekuwa moto wa kuotea mbali michumani akiiwajibikia Juventus na anapewa umuhimu mkubwa katika kufikisha ndoto ya Juventus katika fainali za dimba hilo.

    Amesema kuwa atahakikisha atalinda lango lake na kutotoa mwanya kwa wapinzani kutikisa nyavu zake. Wadadisi wa masuala ya soka tayari wameanza kuweka imani yao kwa uwezo wa Buffon wa kuikingia kifua Juve kutokana na balaa la mashuti ya maangamizi kutoka hasa kwa mshambuliaji hatari wa Real, Christiano Ronaldo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako