• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi wa klabu ya Everton yupo Tanzania kwa maandalizi ya mchezo wao dhidi ya mshindi wa SportPesa Super Cup

    (GMT+08:00) 2017-06-02 11:22:28

    Mkurugenzi wa klabu ya soka ya Everton ya nchini Uingereza, Robert Elstone aliyetua jijini Dar es salaam Jumatano hii kwaajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Julai 13 dhidi ya mshindi wa SportPesa Super Cup, jana alipata fursa ya kutembelea Uwanja wa Taifa na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wao. Ujio wa klabu hiyo iliyoshika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi ya EPL 2016/17, ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kwaajili ya msimu ujao wa ligi.

    "Tunafurahia kuja hapa kuleta timu yetu ya kwanza katika nchi hii na kuwa klabu ya kwanza kufanya hivyo, tunatarajia huu ni mwanzo wa uhusiano wetu kwa kuitambulisha Everton nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Sisi ni klabu ambayo tunajitoa zaidi kwa jamii pamoja na kuibua vipaji vipya, na mambo hayo mawili ni muhimu sana ambayo tungependa kutambulisha hapa Tanzania na Afrika mashariki. Na kwa bahati tumeshuhudia vijana wengi wadogo wakijituma ili kutimiza ndoto zao na Evertone itawezesha kufanya ndoto zao zitimie. Ni wazi kwamba wenyeji wanapenda sana soka kwani nimevutiwa baada ya kuona vijana wadogo wakisakata kabumbu la kuvutia, na unaweza kuona kwamba wanajituma na tunajua kuwa vipaji vipo hivyo kama tutaweza kuibua na kuendeleza vipaji hivyo itakuwa jambo zuri sana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako