• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi kusaidia Rwanda na kuhimiza ujenzi wa utandawazi wa reli kwenye eneo hilo

    (GMT+08:00) 2017-06-02 18:41:29

    Gazeti la The New Times la Rwanda jana liliripoti kuwawataalamu wa Rwanda wanaona reli ya SGR ya Mombasa hadi Nairobi iliyojengwa na kampuni ya China itainufaisha Rwanda na kuhimiza ujenzi wa utandawazi wa reli kwenye eneo hilo.

    Msimamizi wa taifa wa Rwanda wa mradi wa utandawazi wa eneo la kaskazini alisema uzinduzi wa reli hiyo ni mafanikio makubwa, ambayo ni sehemu ya mpango wa kujenga reli ya SGR kwenye eneo hilo, pia ni hatua kubwa iliyopigwa katika kutimiza lengo la mwisho la utandawazi wa reli, na kupunguza ugumu wa kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga utandawazi wa reli. Alisema reli ya SGR ya Mombasa hadi Nairobi itapunguza gharama ya usafirishaji na kufanya biashara, pia ni maendeleo makubwa kwa eneo hilo.

    Naye Mkurugenzi wa taifa wa Rwanda wa shirika la kuhimiza biashara la eneo la Afrika Mashariki alisema, reli hiyo sio tu itapunguza gharama ya usafirishaji na kufanya biashara, bali pia itasaidia kupunguza bei za bidhaa na kupunguza tishio kwa wawekezaji wa utandawazi wa reli katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako