• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika inahitaji dola bilioni 100 kila mwaka ili kufadhili miundo mbinu

    (GMT+08:00) 2017-06-02 19:00:51

    Deni ya nchi nyingi barani Afrika linatarajiwa kuendelea kupanda huku serikali zikiendelea kukopa kufadhili miradi ya miundo mbinu.

    Wataalam wa maswala ya fedha wanasema miradi inahitaji fedha nyingi ni pamoja na, uchukuzi, maji na kawi.

    Lakini hata hivyo ripoti mpya ya benki ya dunia inaonyesha kwamba ni ushiriki wa sekta ya kibinafsi tu ambayo itaweza kusaidia nchi hizo kupunguza mwanya wa miundo mbinu.

    Makadirio ya benki ya dunia yanaonyesha kwamba nchi za chini mwa jangwa la Sahara zinahitaji dola bilioni 100 kila mwaka kuwekeza kwenye miradi ya miundo mbinu ili kukuza uchumi kwa angalau asilimia 2.6 kwa mwaka.

    Lakini nchi hizo zinaweza tu kfadhili asilimia 50 ya fedha hizo na kutegemea mikopo kufikisha dola bilioni 100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako