• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda :Wakulima Rwanda kunufaika na kiwanda cha kusindika chakula

    (GMT+08:00) 2017-06-02 19:01:57

    Wakulima nchini Rwanda wanatarajiwa kunufaika na kiwanda cha kusindika bidhaa za chakula kilichoanzishwa hivi karibuni mjini Kigali.

    Wakurungezi wa kiwanda hicho wamesema watanunua mali ghafi zake moja kwa moja kutoka kwa wakulima hatua mbayo itainua kiuchumi. Hata hivyo wamesema wakulima nchini humo bado hawatoshelezi mahiytaji ya viwanda kwani kiwango cha uzalishaji ni cha chini.

    Kiwanda hicho, Africa Improved Foods ni mradi wa serikali ikishirikiana na washirika wengine wanne wa kimataifa yakiwemo Royal DSM, benki ya maendeleo ya Uholanzi.

    Mwaka huu kiwanda hichokinatarajia kuzalisha hadi tani 35,000 za bidhaa za chakula. Lakini ili kufikia lengo hilo kitahitaji tani 23,000 za mahindi na 7,000 za soya

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako