• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wanaopata huduma ya umeme Tanzania yaongezeka

    (GMT+08:00) 2017-06-02 19:02:36

    Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania imesema upatikanaji wa umeme nchini humo umeimarika na sasa asilimia 32.8 ya wananchi wanapata huduma hiyo ikilinganishwa na asilimia 30 ya walioipata mwaka 2015/16.

    Kadhalika, Wizara imeweka wazi mikakati yake kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia miradi takribani 11 inayotekelezwa iliyo katika hatua mbalimbali za kukamilika inayotarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 2,277; huku vijiji 3,559 vikitarajiwa kupatiwa umeme katika mwaka ujao wa fedha.

    Hayo yalisemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati akiwasilisha bungeni Dodoma jana Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa niaba ya waziri ambaye hajateuliwa na Rais John Magufuli.

    Mwijage aliwasilisha hotuba ya bajeti hiyo baada ya uteuzi wa Waziri Profesa Sospeter Muhongo kutenguliwa na Rais siku kadhaa kabla ya kusomwa kwa bajeti hiyo. Hadi Machi mwaka huu, Wizara hiyo imefikisha huduma hiyo kwa asilimia 67.5 ya wananchi ikilinganishwa na asilimia 40 iliyofikiwa Aprili mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako