• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kampuni za simu ambazo hazijajindikisha kwa soko la hisa kufutiwa leseni zao

    (GMT+08:00) 2017-06-02 19:02:55

    Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) imetakiwa kufuta kampuni za simu za mkononi zote ambazo hazitaki kujiandikisha katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

    Rais wa Tanzania John Magufuli aidha, amezitaka kampuni mbalimbali kujisajili katika mfumo wa ukusanyaji kodi za serikali kwa njia ya kielektroniki, aliouzindua jijini Dar es Salaam jana, mfumo unaosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

    Alisema kituo hicho kilichoanza kazi Oktoba mwaka jana, mwitikio wa kujiunga sio mkubwa, ambapo ni kampuni tatu pekee ambazo zimejiunga na alihimiza zingine kujiunga. Rais Magufuli alisema kwa kutumia kituo hicho, makusanyo ya kodi hayatakuwa na malalamiko tofauti na huko awali kulikuwa na malalamiko kwa wakusanya kodi na pia walipa kodi wakidai kuongezewa viwango.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako