• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ahudhuria mkutano wa 19 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-06-03 15:46:50

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, mwenyekiti wa baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Claude Juncker wameongoza kwa pamoja mkutano wa 19 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya katika makao makuu ya baraza la Ulaya jana asubuhi huko Brussels.

    Bw. Li Keqiang amesema China inatilia maanani uhusiano kati ya China na Ulaya, na kuunga mkono nchi za Ulaya kufuata njia ya utandawazi kwa kujitegemea. China inatarajia mkutano huo utatoa ishara nzuri kwamba uhusiano kati ya China na Ulaya utaendelea kuimarishwa, ili kukabiliana na hali ya mabadiliko duniani.

    Baada ya mkutano huo, viongozi wa China na Ulaya wameshuhudia usaini wa nyaraka zaidi ya 10 za ushirikiano katika mambo ya uwekezaji, hakimiliki, forodha na sayansi na teknolojia, na kuzindua alama za "mwaka wa rangi ya kibuluu kati ya China na Ulaya" na "mwaka wa utalii kati ya China na Ulaya".

    Siku hiyo Bw. Li Keqiang pia amekutana na mfalme Philippe Leopold Louis Marie wa Ubelgiji na waziri mkuu Bw. Charles Michel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako