• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Niger akutana na mjumbe wa taifa wa China

    (GMT+08:00) 2017-06-04 16:29:49

    Rais Mahamadou Issoufou wa Niger amekutana na mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Yong mjini Niamey.

    Bw. Wang amesema China itashirikiana na Niger kutekeleza matokeo ya mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Johannesburg Afrika Kusini, kufanya ushirikiano wa kunufaishana kwenye msingi wa hali ya kuaminiana katika mambo ya kisiasa, urafiki kati ya wananchi wao, na uchumi unaosaidiana. China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na Niger katika mambo ya mawasiliano, umeme, nishati, kilimo na matibabu, na kuisaidia nchi hiyo iwe na uwezo wa kupata maendeleo endelevu kwa kujitegemea.

    Katika ziara yake nchini Niger Bw. Wang Yong pia amekutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Brigi Rafini, spika wa bunge Bw. Ousseini Tini, na kushuhudia usaini wa nyaraka mbalimbali zikiwemo makubaliano ya ushirikiano wa uchumi na teknolojia kati ya nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako