• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya Riadha ya Diamond Ligi, Wakenya kutoana jasho

    (GMT+08:00) 2017-06-05 08:16:14

    Wakenya Nicholas Bett na Boniface Mucheru watawania ubingwa wa mbio za mita 400 kuruka viunzi katika duru ya 5 ya Riadha za Diamond League hapo Juni 15 nchini Norway.

    Bingwa wa Dunia mwaka 2015 Bett na mshindi wa medali ya fedha katika Olimpiki mwaka 2016 Mucheru watakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mfalme wa Olimpiki, Kerron Clement wa Marekani na bingwa wa Ulaya, Yasmani Copello kutoka Uturuki.

    Tangu ashinde taji la dunia jijini Beijing nchini Uchina mwezi Agosti mwaka 2015, Bett hajakuwa na wakati mzuri.

    Bett, Mucheru na Clement walikutana katika duru ya kwanza msimu huu jijini Doha nchini Qatar mnamo Mei 5. Clement alimaliza katika nafasi ya pili kwa sekunde 48.44.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako