• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la IS latangaza kuwajibika na shambulizi la London

    (GMT+08:00) 2017-06-05 09:57:32

    Habari kutoka Shirika la habari la Uingereza BBC zinasema kundi la Islamic State limetangaza kuwajibika na shambulizi la kigaidi lililotokea jumamosi mjini London na kusababisha vifo vya watu 7 na wengine 48 kujeruhiwa.

    kundi la IS limetangaza kwenye tovuti yake kuwa wapiganaji wa kikosi cha usalama cha IS ndio waliofanya shambulizi mjini London.

    Polisi wa Uingereza wamethibitisha kuwakamata watu 12 kuhusiana na shambulizi hilo, na msako dhidi ya washukiwa wengine na uchunguzi bado unaendelea.

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema Uingereza inapaswa kuangalia upya sera zake dhidi ya ugaidi ili kuhakikisha idara za usalama na polisi wana nguvu na mamlaka ya kutosha. Pia amesisitiza kuwa, uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 8 utafanyika kama ilivyopangwa.

    Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa salamu za pole kwa Uingereza na kusema dunia nzima inapaswa kushirikiana zaidi katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako