• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AfDB's itatumia sh trilioni 1.2 ili kuboresha upatikanaji wa umeme Afrika

    (GMT+08:00) 2017-06-05 20:22:21
    Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatumia sh trilioni 1.2 ili kuboresha upatikanaji wa umeme kwa watu zaidi ya milioni 350 Afrika katika kipindi cha miaka mitano.

    Upatikanaji wa umeme Afrika ni moja wapo ya mipango ilipewa kipaumbele na Benki ya Maendeleo ya Afrika nchini ya mkakati wa miaka kumi yake.

    Karibu miradi 50 ilipitishwa katika sekta ya nishati mwaka 2016 na Bodi ya Wakurugenzi.

    Upatikanaji wa umeme bado ni changamoto na benki imedhamiria kubadili mwenendo.

    Pamoja na Umoja wa Afrika, ilikaribisha Mpango wa Nishati Mbadala Afrika ambayo imevutia Sh bilioni 1 katika ahadi za uwekezaji kutoka nchi za G7.

    Umeme ni ghali zaidi nchini Kenya ikilinganishwa na nchi zengine katika bara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako