• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Shirikisho Barani Afrika: Al-Ahly yawapiga Waydad Athletic Club nayo ZESCO yaitandika LIBOLO

    (GMT+08:00) 2017-06-06 08:19:04

    Timu ya Al Ahly SC ya Misri imeichapa mabao 2-0 Wydad Athletic Club ya Morocco katika mchezo wa kundi D ligi ya mabingwa Afrika uliofanyika uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri.

    Moamen Zakaria aliipatia Al Ahly bao dakika ya 24 na Junior Ajayi dakika ya 79 na kuifanya timu hiyo kuongoza kundi lake ikifikisha pointi 7 sawa na Zanaco ya Zambia, inayozidiwa wastani wa mabao na Wamisri hao.

    nayo ZESCO United imepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Recreativo Desportivo Do Libolo katika mchezo wa kundi C wa kombe la Shirikisho Afrika mchezo uliochezwa uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola Zambia.

    ZESCO sasa wanaongoza kundi C baada ya Smouha na El Hilal El Obeid kutoka sare ya 1-1. Mechi zijazo zitachezwa Juni 20 wakati ZESCO itakapoifuata Clube Recreativo Desportivo do Libolo.

    Matokeo ya mechi zingine TP Mazembe imetoka sare ya 2-2 dhidi ya Superport United.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako