• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto laki moja wako hatarini kutokana na mapigano makali magharibi mwa Mosul, Iraq

    (GMT+08:00) 2017-06-06 10:35:23

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa taarifa ikisema watoto laki moja magharibi mwa Mosul nchini Iraq wako hatarini wakati mapigano kati ya jeshi la Iraq na kundi la Islamic State kwenye eneo hilo yanapamba moto. Tahadhari hiyo imekuja wakati vikosi vya serikali ya Iraq vikiungwa mkono na muungano wa kimataifa wa kupambana na kundi la IS vinafanya mashambulizi makubwa ya kuwaondoa wapiganaji wa kundi hilo kutoka kwenye ngome yao magharibi mwa Mosul, ambako maeneo kadhaa likiwemo eneo kongwe la mji huo, bado yanadhibitiwa na kundi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako