• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Luo Junyuan kusaidia watu wa mji wa Jing Gangshan kuondoa umaskini

    (GMT+08:00) 2017-06-06 17:50:26

    Mji wa Jing Gangshan uko katika eneo la mlima wa Luoxiao ambalo kati ya mkoa wa Jiangxi na Hunan. Ni mji wenye rasilimali nyingi za wanyama, miti na una hali ya hewa nzuri. Lakini kutokana na mji huo kuwa katika eneo la milimani, maendeleo yake yameathiriwa. Eneo hilo lilikuwa eneo la maskini zaidi nchini China kutokana na matatizo ya usafiri, na msingi dhaifu wa uchumi. Fadhili Mpunji na maelezo zaidi kuhusu juhudu za mji huo kuondokana na umaskini.

    Mwaka 2014, familia 4734 na watu 17079 walitajawa kama watu maskini ambao ni asilimia 13.8 ya idadi ya jumla ya watu wa mji huo. Hii ina maana kuwa, pato la wastani la watu hao kwa mwaka lilikuwa ni chini ya yuan 2736.

    Bw. Luo Junyuan ni ofisa maalum wa idara ya kilimo ya mkoa wa Jiangxi aliyetumwa kushughulikia mambo ya umaskini katika kijiji cha Paitou katika mji mdogo wa Xincheng, kaskazini magharibi wa mji huo. Wakati ule, familia 35 na watu 147 waliorodheshwa kuwa ni watu maskini. Tatizo la kwanza linalomkabili Bw. Luo, ni jinsi ya kuanza kazi ya kuondoa umaskini. Aliona, jambo muhimu kabisa la kuondoa umaskini ni kuwahamasisha watu kuwa jasiri, na kuamini kuwa wana uwezo wa kuondoa hali hiyo mbaya.

    Pia ilikuwa muhimu kuzungumza nao kuelewa hali yao halisi. Bw. Luo alitumia miezi miwili hadi mitatu kutembelea kila familia kusikiliza maelezo yao kuhusu hali iliyopo. Pia alizungumza na wakuu wa kijiji hicho kuhusu sera na hali ya ujumla ya kijiji hicho. Bw. Luo alitoa misaada kwa wanakijiji kadri alivyoweza na kupata uaminifu kutoka kwa watu wengi.

    Lakini, kutoa msaada kwa muda si utatuzi wa kudumu wa kuondoa umaskini. Muhimu ni kuhakikisha wanakijiji hao wanapata pato nzuri. Bw. Luo alijadiliana na idara ya kilimo ya mkoa wa Jiangxi kutoa mpango wa maendeleo ya miaka mitatu kwa ajili ya kijiji hicho, ili kutatua kihalisi suala la umaskini wa kijiji hicho. Kwa mujibu wa mpango huo, Bw. Luo ameongoza kukarabati mabwawa ya samaki, kujenga bustani ya matunda na mboga, na kituo cha ufugaji. Pia amepata mkopo wa yuan milioni 2.2 kuboresha mashamba ya mpunga ili kuongeza uzalishaji kwa mara moja. Kutokana na hatua hizo, Bw. Luo amesaidia familia maskini zote 35 kuongeza mapato.

    Mwaka 2016, kazi ya kuondoa umaskini katika kijiji hicho ilikaribia kumalizika. Bw. Luo alisema, ataendelea kuimarisha matokeo yaliyopatikana katika kuondoa umaskini na kuzuia watu wasirudi kwenye umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako