• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia:Ethiopian Airlines yateuliwa kuwa kampuni bora ya ndege Afrika

    (GMT+08:00) 2017-06-06 18:41:39

    Kampuni ya ndege ya Ethiopian Ailines imeteuliwa kuwa kampuni bora ya ndege mwaka 2016-17 katika kongamano la kila mwaka la huduma za ndege Afrika.

    Kampuni hii imetuzwa kutokana na mchango wake wa maendeleo ya safari za angani mbali na kuweka rekodi ya kuingiza faida nyingi .

    Taarifa iliyotolewa na shirika la Fedha Afrika la ndege Afrika nchini Afrika Kusini imeelezea kwamba uongozi wa Ethiopian Airlines umefanikiwa kuimarisha viwango vya huduma kwa wateja pamoja na ulipaji bora wa wafanyikazi.

    Meseret Bitwe afisa mkuu wa fedha wa kampuni hiyo amesema tuzo hiyo waliyopewa kwa mara ya pili mtawalia inawapa motisha ya kuzidisha juhudi za kuunganisha Afrika na nchi za ulaya katika ipango ya biashara na utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako