• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Serikali kuwafikishia huduma ya umeme wakenya milioni 1

    (GMT+08:00) 2017-06-06 18:43:02
    Serikali ya Kenya inalenga kuwafikishia huduma ya umeme wakenya milioni 1 katika mda wa wiki tatu.

    Waziri wa fedha Henry Rotich amesema wizara yake imetenga fedha kupitia kwa bajeti ya ziada ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wakenya na kuinua uchumi wao kupitia kwa shughuli za biashara.

    Aidha kufikia mwezi Disemba serikali inatarajia kufikisha huduma hiyo kwa wakenya wengine laki 5 .

    Wateja watatakiwa kulipa shilingi elfu 15 pekee tofauti na elfu 60 za hapo awali ili kuunganishiwa gogo la kusambaza transmitter za umeme huo.

    Kampuni ya Kenya Power imesema mradi huo wa serikali umewasaidia wakenya wengi maskini waliokosa uwezo wa kifedha kupata umeme katika nyumba zao.

    Shilingi bilioni 20 ziliztengwa kwa ajili ya umeme kufikishwa katika eneo la Suswa ,Naiobi,Momabasa hadi Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako