• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Kuwait yatoa mkopo wa dola milioni 51 Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-06-06 18:43:21

    Serikali ya Kuwait imetoa mkopo wa wa Dola za Marekani milioni 51 (sawa na takribani Sh bilioni 110), kwa ajili ya kujenga barabara ya Chaya - Nyahua mkoani Tabora yenye urefu wa kilometa 85.

    Barabara hiyo itaunganisha mawasiliano ya barabara kati ya mkoa wa Singida na Tabora.

    Rais Magufuli amepokea mkopo huo kupitia Balozi wa Kuwait hapa nchini, Jasem Ibrahim Al Najem .

    Aidha, Rais Magufuli aliishukuru Serikali ya Kuwait kwa kutoa Dola za Marekani milioni 50 kwa ajili ya kuikarabati Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja iliyopo Zanzibar. Pia aliiomba Serikali ya Kuwait kuweka alama ya kumbukumbu ya uhusiano wake na Tanzania kwa kusaidia ujenzi wa barabara za makao makuu ya nchi mjini Dodoma.

    Kwa upande wake, Balozi wa Kuwait hapa nchini, Jasem Ibrahim Al- Najem alielezea kufurahishwa kwake na uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya nchi yake na Tanzania. Alimhakikishia Rais Magufuli kuwa Kuwait ipo tayari wakati wowote, kuunga mkono juhudi za maendeleo kulingana na vipaumbele vya Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako