• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TFF yapeleka maombi rasmi kuiombea Zanzibar uanachama wa shirikisho la soka Duaniani (FIFA)

    (GMT+08:00) 2017-06-07 08:16:08

    Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limepeleka maombi kwenye shirikisho la soka duniani (FIFA) kuiombea Zanzibar kuwa mwanachama wa shirikisho hilo.

    Afisa muandamizi anayeshughulikia ruzuku wa TFF Derek Murusuri alikutana na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na kumueleza mipango inayoandaliwa na TFF kuhakikisha inaipatia nakala Zanzibar kuthibitisha hatua zilizochukuliwa.

    TFF inaendelea na mikakati ya kukusanya vijana wenye vipaji kwa lengo la kuwaandaa kupitia mashindano mbalimbali ya kitaifa, kikanda ili kupata timu imara itakayoshiriki kombe la dunia mwaka 2026.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako