• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa China yawakamata watuhumiwa wa matumizi haramu ya vifaa vya kijasusi

    (GMT+08:00) 2017-06-07 10:17:14

    Polisi wa mji wa Ganzhou, mkoani Jiangxi, China wamewakatama watu watatu kwa tuhuma za kutumia kiharamu vifaa vya kijasusi.

    Kwa mujibu wa polisi, watuhumiwa hao watatu waliingia kwenye kiwanda fulani cha mji wa Ganzhou na kutumia saa ya kupigia picha na kifaa cha kunasa sauti kuiba data zinazohusiana na siri za kibiashara na kuzitoa kwa mashirika husika ya nchi za nje, ili kujipatia fedha.

    Watuhumiwa hao waliingia katika viwanda kadhaa vilivyolengwa kote nchini, kupiga picha na video kuhusu mchakato wa utengenezaji, na nyaraka za ndani za viwanda hivyo na kuzitoa kwa mashirika ya nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako