• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: serikali kusafirisha nje mafuta ghafi mara tatu kwa mwaka

    (GMT+08:00) 2017-06-07 19:33:02
    Kenya litasafirisha mafuta ghafi kutoka Turkana mara tatu kwa mwaka na mafuta lazima ikusanywe kwa muda wa miezi kadhaa ili kuweza kujaza meli.

    Mwezi huu nchi inatarajiwa kusafirisha mapipa 2,000 kwa siku kutoka Turkana kwa njia ya barabara hadi kwa eneo la kuhifadhia matenki Mombasa.

    Katibu mkuu wa mafuta bw, Andrew Kamau amesema mafuta yatahifadhiwa katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Mariakani kwa kati ya miezi tatu na nne.

    Uzalishaji mdogo wa mafuta ghafi unatarajiwa kuendelea hadi mwaka 2021 wakati Kenya inatarajia kuwa na bomba yake yenyewe.

    Hivi sasa Tullow imehifadhi zaidi ya mapipa 70,000 ya mafuta katika eneo la Lokichar katika maandalizi ya mpango wa mauzo ya nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako