• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vodacom kuvunja rekodi ya mauzo ya DSE soko la awali

    (GMT+08:00) 2017-06-07 19:33:28

    WAWEKEZAJI zaidi ya 40,000 wamevutiwa na hisa za Vodacom Tanzania PLC zinazoendelea na mchakato wa kuingia sokoni.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, amesema hisa hizo zitakuwa za kihistoria na zitavunja rekodi kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa miaka 19 tangu kuanzishwa kwake.

    Hii imechangia kwa kiasi kikubwa malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutaka kuona Watanzania wanakuwa wamiliki wa kampuni kubwa zinazofanya biashara nchini.

    Katika taarifa yake, Ferrao amesema, Vodacom Tanzania PLC inajivunia kuwa kampuni ya mawasiliano inayoongoza Tanzania na ndiyo kampuni ya kwanza kutimiza masharti ya Bunge la Tanzania ya kutaka makampuni zote za simu za mkononi kuorodhesha hisa zake kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako