• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tetesi za usajili wa wachezaji mbalimbali wa soka

    (GMT+08:00) 2017-06-08 08:34:38

    Na sasa ni habari za usajili wa wachezaji zilizovuma jana Jumatano. Habari za chinichini zinadai kuwa klabu ya Arsenal imeshindwa kuhusiana na suala la mkataba mpya wa Alexis Sanchez na sasa mshambuliaji huyo wa klabu ya Arsenal yuko mbioni kujiunga na klabu ya Manchester City ambao wameshafanya mazungumzo naye ya chini chini.

    Manchester United nao kwa upande wao inaonekana ni kama wameshashinda vita ya kumbakiza David De Gea kwa mara nyingine kwani inasemekana klabu ya Real Madrid wameona ni ngumu sana kumnunua golikipa huyo na wameamua kuachana na mpango huo.

    Baada ya kuweka wazi kwamba mwishoni mwa msimu huu ataondoka Real Madrid sasa mlinzi wa kati wa timu hiyo Pepe inadaiwa kwamba huenda katika msimu ujao wa ligi tukamuona katika ligi kuu nchini Ufaransa ambako anakaribia kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya PSG.

    Kocha wa Chelsea Antonio Conte anajipanga kutoa kiasi cha pesa pamoja na mchezaji mmoja kwa Juventus ili kuweza kumpata Leonardo Bonucci, Conte atalazimika kuwapa Juventus kiasi cha euro milioni 48 na Nemanja Matic ili kumnunua Bonucci, kama Chelsea hawatatoa mchezaji mchezaji itawabidi watoe euro milioni 60.

    Michy Batshuayi ameweka wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu ya Chelsea baada ya kukosa nafasi ya kucheza. Naye Steven Gerrard kwa mara ya kwanza nusura ajiunge na kocha Jose Mourinho, Gerrard amesema kuna wakati Jose Mourinho alipokuwa akiifundisha Chelsea na baadae wakati anaifundisha Real Madrid alikaribia kujiunga na kocha huyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako