• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taifa Stars yarudi Dar ikiwa na ari ya kuwashinda Lesotho

    (GMT+08:00) 2017-06-08 08:35:19

    Jana timu ya taifa 'Taifa Stars' ilirudi Dar ikitokea Misri ambako ilikuwa kwenye kambi ya wiki moja ikijiandaa kwa mchezo dhidi ya Lesotho mechi ambayo ni ya kwanza kuwania kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2019.

    Kocha wa Stars Salum Mayanga amsema madaktari wa timu hiyo walishauri beki wake wa kushoto na klabu ya Simba Mohamed Hussein 'Tshabalala' asifanye mazoezi kwenye kambi ya nchini Misri.

    Mohamed Hussein alipata majeraha kwenye mechi ya fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup wakati Simba ikipambana na Mbao FC kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma. Hakuweza kuendelea na mchezo na benchi la ufundi la Simba likalazimika kumtumia Abdi Banda kuziba nafasi yake.

    Mayanga pia amesema kila kitu kilikwenda vizuri nchini Misri na walipata kila walichohitaji kwa ajili ya mazoezi yao na anatumai baada ya kurudi watafanya mazoezi kwa siku mbili leo watafanya mazoezi usiku na kesho asubuhi ili kuweza vizuri siku ya Jumamosi, na kwa kujituma na kwamba anaamini wawatashinda Lesotho."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako