• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Promota Eddie Hearn amfagilia bondia Wladimir Klitschko kwenye pambano la marudiano dhidi ya Anthony Joshua

    (GMT+08:00) 2017-06-08 08:36:08

    Promota, Eddie Hearn anaamini bondia, Wladimir Klitschko kama atakubali mchezo wa marudiano dhidi ya Anthony Joshua basi mchezo huo utakuwa mgumu kwani atakuwa ni mwenye kujiamini zaidi.

    Joshua, ambaye alimpiga Klitschko katika uwanja wa Wembley mwezi Aprili, na Promota wake wameridhia kuchezwa kwa mchezo huo wa marudiano baina ya mabondia hao wawili wa uzito wa juu lakini ufanyike mwezi Desemba.

    Hearn ambaye ni promota wa ngumi aliuambia mtandao wa Sky Sports News HQ kwamba huo utakuwa mchezo wa kukata na shoka kwa sababu Anthony Joshua ataingia katika mchezo huku akiwa na kumbukumbu za kuumizwa katika mchezo uliopita wakati, Wladimir Klitschko pia akiwa na kumbukumbu za kupoteza mchezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako