• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mayweather kuzichapa na Spika wa baraza la wawakilishi la Nigeria kwenye pambano la hisani

    (GMT+08:00) 2017-06-08 08:36:30

    Bondia mstaafu na bosi wa 'The Money Team' (TMT), Floyd Mayweather Jr anatarajia kutua nchini Nigeria Juni 12 hadi 14 mwaka huu na kuzichapa na Spika wa baraza la wawakilishi nchini humo, Yakubu Dogara kwenye pambano la hisani.

    Akizungumza na waandishi wa habari mapema wiki hii mjini Lagos Mwenyekiti wa Tettrazzini Group of Companies, Kampuni mama ya Zzini Media ambao ni waandaaji wa ziara hiyo, Bw. Donatus Okonkwo amesema Mayweather atazichapa na Mh. Yakubu Dogara katika pambano la hisani lililoandaliwa na Baraza la wawakilishi (Bunge) nchini humo.

    Naye Floyd Mayweather amethibitisha taarifa hizo kwa kusema atakuwepo nchini humo june 12 hadi 14, huku mtandao wa Guardian ukiandika kuwa bondia huyo licha ya pambano hilo atatembelea mapango ya Ogbunike yaliyo kusini mwa nchi hiyo ambayo ni kivutio kikubwa cha watalii.

    Mayweather mwenye miaka 40 hajawahi kupoteza pambano lolote katika historia ya mchezo huo wa masumbwi akiwa amecheza mapambano ya ubingwa 46 na kushinda yote huku akiwa na Knockout 26 tangu mwaka 1996 hadi 2015 alipotangaza kustaafu, atatembelea miji ya Lagos, Anambra, Akwa Ibom na Abuja kabla ya kuelekea nchini Ghana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako