• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gerard Pique aendeleza mipasho yake dhidi ya Real Madrid

    (GMT+08:00) 2017-06-08 08:37:20

    Baada ya Real Madrid kufanikiwa kutetea ubingwa wa champions league wiki iliyopita walipongezwa na kila mtu ikiwemo klabu ya Barcelona ambao ni waajiri wa mlinzi wa kati Gerard Pique.

    Lakini sio Klabu nzima yenye moyo safi wa kuipongeza Madrid kwani kwa Pique ni tofauti sana na anaona hakuna kitu walichofanya Madrid ambacho hakiwafanyi kuwa bora kuliko wao.

    Akiongea na kituo kimoja cha habari nchini Hisapania Pique amesema Real Madrid hawawezi kuigusa Barcelona hata kidogo na kwamba haiwezekani kufananisha walichoshinda katika miaka ya hivi karibuni na kile ambacho tumeshinda wao.

    Hii si mara ya kwanza kwa Pique kuishambulia Real Madrid kwani kama itakumbukwa hata katika mchezo kati ya Real Madrid na Bayern Munich Pique aliiponda Real Madrid kwa kuwaambia wanabebwa sana na waamuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako