• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga ripoti ya Marekani kuhusu nguvu ya kijeshi ya China

    (GMT+08:00) 2017-06-08 08:49:50

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Bw. Wu Qian amesema, China inapinga kithabiti ripoti kuhusu maendeleo ya nguvu ya kijeshi ya China iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani, ambayo imetoa tathmini bila ya msingi, kutilia chumvi "tishio la kijeshi la China" na kutoa maoni bila kujali hali halisi kuhusu hali ya mlango wa bahari wa Taiwan.

    "China siku zote inashikilia mkakati wa kujiendeleza kwa amani, na kufuata sera ya kujilinda ya ulinzi wa taifa. Katika miaka ya hivi karibuni, jeshi la China limetekeleza majukumu katika nchi za nje kwenye operesheni mbalimbali ikiwemo ulinzi wa amani, ulinzi wa misafara ya meli na uokoaji maafa, kutoa bidhaa nyingi zaidi za usalama wa umma, hatua ambazo zimepata pongezi za jumuiya ya kimataifa. China haitapanua jeshi lake, na wala haitafuti kudhibiti nchi za nje, na siku zote inaendelea kuwa nguvu thabiti ya kulinda amani ya dunia."

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying pia amepinga ripoti hiyo, akisema China inaitaka Marekani iheshimu kanuni za taarifa tatu za pamoja za China na Marekani na sera ya China moja, kuacha kuiuzia silaha Taiwan, kusitisha uhusiano wa kijeshi na Taiwan na kushughulikia kwa makini masuala yanayohusiana na Taiwan, ili isije ikauharibu uhusiano kati ya Marekani na China na utulivu wa mlango bahari wa Taiwan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako