• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magaidi sita wauawa katika mashambulizi ya kigaidi Iran

    (GMT+08:00) 2017-06-08 09:22:02

    Shirika la habari la Iran limesema magaidi sita wamepigwa risasi au kujilipua wakati walipofanya mashambulizi katika makao makuu ya bunge la Iran na kaburi la Imamu Khomeini.

    Magaidi wanne waliojifanya wanawake waliingia kwenye jengo la bunge la Iran jana mchana na kuwafyatulia risasi polisi baada ya kuzuiliwa, mmoja wao alijilipua na kufa papo hapo na wengine watatu wakauawa kwa kupigwa risasi na kikosi maalumu.

    Wakati huo huo magaidi wawili walijipenyeza kwenye kaburi la Imamu Khomeini na kufyatua risasi, mmoja wao alijilipua na mwingine aliuawa kwa kupigwa risasi wakati wakipambana na kikosi cha walinzi.

    Kundi la IS limetangaza kuhusika na mashambulizi hayo yaliyosababisha vifo vya watu 12 na wengine 42 kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako