• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkoa wa Qinghai wazingatia kuboresha maisha ya watu na kuondoa umaskini

    (GMT+08:00) 2017-06-08 17:56:06

    Mkoa wa Qinghai liko uwanda wa juu magharibi mwa China. Hali ya maendeleo ya mkoa huo inakabiliwa na changamoto nyingi. Asilimia 90 ya watu maskini wanaishi katika eneo la milimani au maeneo yenye ukame. Ni vigumu kuwasaidia watu wa huko kuondokana na umaskini kutokana na maafa mengi, na kuwa na msingi dhaifu wa uchumi.

    Kwa muda mrefu, serikali ya mkoa wa Qinghai imekuwa inatafuta njia nzuri ya kuondoa umaskini na kupata maendeleo. Imejitahidi kutumia vizuri fedha kutatua masuala ya umma kama vile elimu, ajira, na matunzo ya wazee.

    Mkurugenzi wa idara ya maendeleo na kuondoa umaskini ya Qinghai, Bw. Ma Fengsheng amesema, maofisa wa serikali wameweka kipaumbele kuboresha maisha ya watu. Kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2016, wamesaidia watu milioni 1.165 kuondoa umaskini na kupunguza kiwango cha umaskini kutoka asilimia 37.6 hadi 10.3. Serikali ya mkoa huo imetumia watu wapatao elfu 10 kutambua sababu za watu wanaokumbwa na umaskini na kupata usahihi wa asilimia 99.24 katika utambuzi wa maskini.

    Kutokana na tofauti kubwa zilizopo, serikali ya mkoa wa Qinghai imetafuta njia pekee mwafaka ya kukabiliana na matatizo hayo. Bw. Ma amesema, mkoa wa Qinghai ni eneo muhimu la uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo maalum kwenye uwanda wa juu nchini China. Serikali inachukua fursa hiyo kutilia maanani maendeleo ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo maalum na utengenezaji wa bidhaa za kilimo, ili kuhimiza watu maskini kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato. Katika eneo la mifugo, serikali inawasaidia wafugaji kukodisha malisho yao ili kuongeza uzalishaji, kutoa nafasi zaidi ya ajira na kuongeza mapato.

    Serikali ya mkoa huu imeanzisha mashirika madogo madogo vjijini kuwasaidia wakulima kutunza mazingira, kuhimiza maendeleo ya kilimo na kuongeza mapato yao. Pia imewasaidia kushirikiana na makampuni ya kikanda kuendeleza mazao ya kilimo na mifugo maalum, na kuhakikisha soko la bidhaa zao.

    Meneja wa kampuni ya maziwa, Bibi Guan Queji amesema, kutokana na sera nzuri ya serikali, amenufaishwa sana katika kupata mikopo na kuunda kampuni. Mwaka 2004, pato lake lilikuwa ni yuan 400 hivi kwa mwezi. Mwaka jana, pato la kampuni yake limefikia yuan milioni 6 kwa mwaka. Amesema, serikali sio tu kwamba imemsaidia kupata mikopo, bali pia imemsaidia kurahisisha uendeshaji wa kampuni kwa kuanzisha mashirika ya wafugaji. Ushirikiano kati ya wafugaji na kampuni yake umeziwezesha mapato ya familia elfu mmoja ya wafugaji kuongezeka kwa yuan elfu 10 kwa mwaka.

    Pamoja na kuwa kazi ya kuondoa umaskini ni suala lenye changamoto nyingi, Bw. Ma Fengsheng ana imani kuwa serikali ya mkoa wa Qinghai inaweza kutimiza lengo la kuondoa umaskini vijijini kabla ya mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako