• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia: Shirika la ndege la Ethiopia lashinda tuzo la shirka bora Afrika

    (GMT+08:00) 2017-06-08 18:52:47
    Shirika la ndege la Ethiopia kwa mara nyingine tena limeshinda tuzo la shirka bora barani Afrika.

    Ni mara ya pili kwa shirika hilo kushinda tuzo hilo linalotolewa kwenye maonyesho ya usafiri wa anga.

    Mwaka huu maonyesho hayo yamefanyika mjini Johannesburg Afrika Kusini.

    Shirika hilo limetambuliwa kwa juhudi zake za upanuzi, kupanda kwa faida na kuchangia ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga barani Afrika.

    Licha ya kuwa na kipindi kigumu kwenye sekta hiyo mwaka hu, mkurungezi wa shirika hilo Meseret Bitew, amesema wamefanikiwa kuboresha huduma na pia kuongezea maeneo zinakosafiri ndege zake.

    Faida ya mwaka 2016 ya shirika hilo imekua kwa asilimia 70 ambako ilipata dola milioni 265 huku wasafiri wakiongezeka kwa asilimia 18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako