• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali ya Tanzania yatoa takwimu za hali ya ukuaji uchumi

    (GMT+08:00) 2017-06-08 18:53:13

    Serikali ya Tanzania imetoa takwimu ikielezea hali ya ukuaji uchumi katika kipindi cha mwaka 2016 na kueleza kuwa kiwango hicho kimeendelea kukua kwa wastani wa asilimia saba ikiwa ni pungufu kidogo ya kile kilichotarajiwa awali.

    Akisoma hotuba ya mwelekeo wa hali ya uchumi wa Taifa bungeni leo Alhamisi, Waziri wa Fedha na Mpango , Dk Philip Mpango amesema makadirio ya awali yalionyesha kuwa uchumi huo ungekua kwa wastani wa asilimia 7.2.

    Amsema hali ya ukuaji uchumi imeendelea kushuhudiwa katika kiwango kilekile cha awali cha asilimia saba na hii imechangiwa na mambo mengi ikiwamo baadhi ya sekta kutofanya vizuri.

    Ametaja baadhi ya sababu hizo kuwa ni pamoja na kushuka wa sekta ya kilimo iliyotarajiwa kukua kwa asilimia 2.9, lakini malengo hayo hayakufikiwa na badala yake yalikuwa kwa asilimia 2.1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako