• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Diego Costa athibitisha kutotakiwa na kocha wake Antonio Conte

    (GMT+08:00) 2017-06-09 09:08:30

    Ule uliotajwa kama ugomvi kati ya Diego Costa na kocha wake Antonio Conte ambao ulitokea katika dirisha lililopita la usajili haujaisha. Ikumbukwe kuwa kulikuwa na tetesi kwamba Costa alilazimisha kuuzwa China jambo ambalo lilimkera Conte na kuamua kumuacha katika mchezo mmoja wa ligi.

    Baadae mambo yalionekana kuwa sawa na Conte akasisitiza hakuna tatizo kati yake na Costa na kwamba mshambuliaji huyo anaipenda Chelsea na hana mpango wa kuondoka na kuanzia hapo taarifa za msuguano kati ya hao wawili zikazimwa na Costa akaendelea kucheza Chelsea na kwa kiwango cha juu kabisa.

    Takribani mwezi sasa umepita tangu Chelsea watwae ubingwa, na Diego Costa ameibuka na kusema kwamba kocha Antonio Conte amemtumia ujumbe na kumuambia hayupo kwenye mipango yake, Costa aliyasema hayo wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Hispania na Colombia.

    Tayari inaonekana Conte amesahau msaada mkubwa wa Costa kwani mabao 20 na assist 3 alizotoa msimu huu zilichangia kwa kiasi kikubwa ubingwa wa Chelsea lakini Conte hana mpango naye tena na tayari ameanza kumtafutia mtu wa kukaa nafasi yake huku Romelu Lukaku akitajwa kuwa mbadala wa Costa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako