• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga yayaaga mashindano ya SportPesa Super Cup

    (GMT+08:00) 2017-06-09 09:10:04

    Yanga imeyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup kufuatia kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-2 na AFC Leopards ya Kenya kwenye mchezo wa nusu fainali.

    Mikwaju ya penati ililazimika kutumika kumpata mshindi atakaefuzu kucheza fainali baada ya dakika 90 kumalizika huku timu hizo zikiwa zimetoka suluhu.

    Golikipa wa Yanga Deogratius Munishi 'Dida' alipangua penati moja ya Marselas Ingotsi lakini golikipa wa AFC Leopard Dennis Shikai aliokoa penati za Said Mussa na Said Juma 'Makapu' wa Yanga.

    Penati mbili za Yanga zimefungwa na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' na Mzambia, Obrey Chirwa wakati kwa upande wa AFC Leopards penati zikifungwa na Bernard Mango, Allan Katerega, Duncan Otieno na Dennis Shikai. Yanga ndio ilikuwa timu pekee iliyofuzu hatua ya nusu fainali baada ya Singida United na Simba kutupwa nje kwenye mechi zao za kwanza za mashindano hayo.

    Timu zote za Tanzania zimetolewa kwa matuta kufuatia kushindwa kufungana ndani ya dakika 90. Singida United ilitolewa na AFC Leopards, Simba wakatolewa na Nakuru All Stars na Yanga wametupwa nje ya mashindano na AFC Leopards.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako