• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NBA: Golden State Warriors yaendelea kuifumba mdomo Cleveland Cavaliers

    (GMT+08:00) 2017-06-09 09:10:27

    Golden State Warriors imeendelea kuinyanyasa Cleveland Cavaliers katika fainali ya tatu ya mchezo wa kikapu wa NBA.

    Katika mchezo huo uliochezwa alfajiri ya kuamkia jana katika uwanja wa Quicken Loans Arena, Golden wameshinda kwa jumla ya vikapu 118 dhidi ya 113 vya Cleverland.

    Mchezaji Kevin Durant ameendelea kuwa nyota wa fainali hizo baada ya kufanikiwa kushinda pointi tatu zikiwa zimebakia sekunde 45 za mchezo huo kumalizika.

    Kwa sasa unasubiriwa mchezo wa mwisho utakaochezwa wikiendi hii ambapo kama Golden itashinda tena ndio itakuwa bingwa mpya wa mchezo huo kwa mwaka huu ambao msimu uliopita ulinyakuliwa na Cleveland Cavaliers.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako