• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya SGR ya Kenya yasafirisha abiria elfu 12 katika wiki ya kwanza

    (GMT+08:00) 2017-06-09 11:04:03

    Kampuni ya reli ya Kenya imesema, hadi kufikia tarehe 7, kwa muda wa wiki moja reli ya SGR iliyojengwa na kampuni ya China imesafirisha abiria karibu elfu 12.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni hiyo, kuanzia Juni 1 hadi 7, tikiti elfu 14 ziliuzwa, tikiti elfu 2 kati ya hizo zilinunuliwa na wajenzi wa reli hiyo, wachina wanaoishi Kenya na wakazi wa huko kama kumbukumbu.

    Habari nyingine zinasema, waziri wa fedha na mipango ya kiuchumi wa Rwanda Bw. Claver Gatete amesema, reli ya SGR kati ya Mombasa na Nairobi iliyozinduliwa hivi karibuni ni muhimu kwa mafungamano ya nchi za Afrika Mashariki.

    Amesema, viongozi wa kanda hiyo wanatilia maanani umuhimu wa ujenzi wa reli ya SGR, ikiwa sehemu ya ushoroba wa kaskazini unaounganisha Kenya na Uganda, Rwanda na Burundi, na Ushoroba wa kati unaoanzia nchini Tanzania kupita nchini Rwanda na kuelekea Burundi, ambayo itapunguza gharama za biashara na gharama za usafirishaji wa watu na bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako