• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kuwasiliana na Pakistan kuhusu Wachina wawili waliotekwa nyara nchini Pakistan

    (GMT+08:00) 2017-06-09 18:34:20

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, idara husika za serikali ya China na ubalozi wa China nchini Pakistan zinafanya juhudi zote kuwaokoa raia wawili wa China waliotekwa nyara na kundi la IS nchini Pakistan tarehe 24 mwezi uliopita.

    Bi Hua amesema serikali ya China na ubalozi wake nchini Pakistan inafanya juhudi zote ili kuwakoa, ingawa Palestina inasema huenda watu hao wameuawa. Amesisitiza kuwa China inapinga kithabiti vitendo vyovyote vya kigaidi, na kuunga mkono juhudi za Pakistan katika kupambana na ugadi na kulinda amani na utulivu nchini humo. China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ikiwemo Pakistan katika mapambano dhidi ya ugaidi ili kulinda amani na utulivu wa kimataifa na kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako